RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Paul Rusesabagina: Sijui nilifikaje Rwanda?

Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.
Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi. NICOLAS MAETERLINCK / BELGA / AFP

Shujaa wa filamu Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina, sasa anadai kuwa aliamini kuwa alikuwa akisafiri kuelekea nchini Burundi kwa mwaliko wa mchungaji, kabla ya kujikuta nchini Rwanda  ambapo alikamatwa na kushtakiwa kwa makossa ya ugaidi, limeripoti shirika la habari la New York Times.

Matangazo ya kibiashara

Kesi ya Rusesabagina ilianza kusikilizwa mapema wiki hii, na siku ya Alhamisi alinyimwa dhamana na mahakama ya Rwanda, na atasalia kizuizini kwa siku 30, upande wa mashtaka ukisema bado unaendelea na uchunguzi wake.

Paul Rusesabagina, raia wa Rwanda anayekumbukwa kwa kuwaokoa zaidi ya Wanyarwanda zaidi ya Elfu Moja katika hoteli moja jijini Kigali alifunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Wakili wake David Rugaza, aliiambia mahakama kuwa mashtaka dhidi ya mteja wake si ya kweli na hastahili kufunguliwa mashtaka hayo na hivyo anastahili kuachiliwa huru.

Rusesabagina ni kiongozi chama cha MRCD ambacho kinashtumiwa kushirikiana na kundi la FLN.