UGANDA-USALAMA

Polisi Uganda yachunguza chanzo cha moto katika Chuo Kikuu cha Makerere

Chuo Kikuu cha Makerere kilianzishwa mwaka 1922 mara ya kwanza kama shule ya ufundi.
Chuo Kikuu cha Makerere kilianzishwa mwaka 1922 mara ya kwanza kama shule ya ufundi. Wikimedia / Eric Lubega and Elias Tuheretze

Moto mkubwa umeteketeza jengo maarufu katika chuo kikuu cha Makarere katika mji mkuu wa Uganda, Kampala. Kufikia sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wameanza uchunguzi  kubaini chanzo cha moto huo ambao naibu kansela wa chuo hicho Profesa Barnabas Nawangwe amesema ni tukio la kushangaza.

Jengo hilo maarufu lililoungua mbalo linafahamika kama Ivory Tower, lenye kuta nyeupe na madirisha ya bluu, ni moja ya majengo yanayotambulisha Chuo hicho maarufu barani Afrika.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa huenda moto huo ulianzia kwenye paa, na baadae kusambaa kwenye sakafu za majengo ya vitengo vya fedha na rekodi za chuo.

Chuo Kikuu cha Makerere kilianzishwa mwaka 1922 mara ya kwanza kama shule ya ufundi.