TANZANIA-ACT-UCHAGUZI-SIASA

Kinara wa upinzani visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad azua gumzo

Bernard Membe amesema amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile.
Bernard Membe amesema amejiunga na chama cha ACT-Wazalendo kama mwanachama wa kawaida lakini yuko tayari kutumikia chama hicho kwa ngazi na namna yoyote ile. Dotto Rangimoto/twitter.com

Joto la uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupanda ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya uchaguzi wake wa tano tarehe 28 mwezi Oktoba tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Kumeibuka mjadala baada ya kinara wa upinzani visiwani Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, kutangaza kumuunga mkono mgombea wa chama kikuu cha upinzani Tundu Lissu badala ya mgombea wa chama chake.

ACT tayari kilikuwa na mgombea wake katika kinyang'anyiro hicho ambaye ni waziri wa mambo ya mje wa zamani wa Tanzania, Benard Membe.

Hatua ya Membe kujiunga na ACT Wazalendo miezi miwili iliyopita ilisisiimua siasa za upinzani nchini. Wakati huo, hakukuwa na uhakika endapo Lissu angerejea Tanzania na kuwania urais kama alivyokuwa ametangaza.

Lissu pia alitumia vizuri fursa ya kufanya kampeni Zanzibar wiki mbili zilizopita. Katika Uwanja wa Kibandamaiti, Unguja, Lissu alitangaza kwamba chama chake kinamuunga kumuunga mkono mgombea urais wa visiwa hivyo katika uchaguzi huu, Maalim Seif.

Upinzani ulikuwa unalilia kuwa na mgombea wa kushindana na rais John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bernard Membe aliyefukuzwa kutoka katika chama chake alikuwa na sifa zote za kuwa kinara wa upinzani.