KENYA-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi yaanza kupungua Kenya

Kenya imeendelea na juhudi za kuzuia kuenea kwa Corona.
Kenya imeendelea na juhudi za kuzuia kuenea kwa Corona. REUTERS/Jackson Njehia

Wizara ya afya nchini Kenya imetanagaza kuwa maambukizi ya Covid-19 yameanza kupungua nchini humo, baada ya idadi ya watu wanaoambukizwa kila siku kupungua kwa wiki kadhaa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Wizara hiyo imeendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua hatua ili kuzuia uwezekano wa kutokea kwa mlipuko wa pili.

Saa 24 zilizopita watu 130 walipatikana na virusi hivyo na kufikisha idadi ya maambukizi kufikia 37, 348 tangu mwezi Machi.

Kenya ni moja ya nchi za Afrika Mashariki ambayo imeendelea kutangaza takwimu za maambukizi, vifo na wagonjwa wanaopona ugonjwa huo hatari wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.