UGANDA-CORONA-AFYA

Uganda yafunga hospitali ya Kapchorwa bada ya kuripotiwa maambukizi zaidi

Wizara ya afya ya Uganda imesema imechukua hatua ili kudhibiti maambukizi zaidi, wakati huu nchi hiyo ikiwa na maambukizi zaidi ya 6,700.
Wizara ya afya ya Uganda imesema imechukua hatua ili kudhibiti maambukizi zaidi, wakati huu nchi hiyo ikiwa na maambukizi zaidi ya 6,700. Badru KATUMBA / AFP

Hospitali ya Wilaya ya Kapchorwa Mashariki mwa Uganda, imefungwa baada ya wafanyakazi 19 kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, kitengo cha kuwazalisha wanawake wajawazito na maabara hayajafungwa ili kutoa huduma za dharura.

Wizara ya afya imesema imechukua hatua hiyo ili kudhibiti maambukizi zaidi, wakati huu nchi hiyo ikiwa na maambukizi zaidi ya 6,700.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya Jane Ruth Acieng, amesema kuelekea kufunguliwa kwa shule mwezi ujao, jitihada zinafanyika kuwapima walimu virusi vya Corona.

Wakati huo huo John Nkengasong, mkuu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuwia magonjwa (ECDC) ameyasifu mataifa ya Afrika kwa kuweza kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Afrika imeshuhudia maambukizi ya corona ya watu milioni 1.4, na vifo 34,000 tangu mwezi wa Machi.

Idadi hiyo ni ndogo sana kuliko ile ya mabara ya Ulaya, Asia na Amerika Kaskazini na Amerika Kusini, huku idadi ya maambukizi ikiendelea kupungua.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.