KENYA-SIASA-USALAMA

Mahakama yasitisha mpango wa kuvunja mabunge yote mawili Kenya

David Maraga (katikati), Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Kenya.
David Maraga (katikati), Jaji Mkuu wa Mahkama Kuu Kenya. Photo: Reuters/Baz Ratner

Mahakama Kuu nchini Kenya, imeagiza kusitishwa kwa mpango wowote wa kulivunja bunge la kitaifa na lile la Senate, baada ya Jaji Mkuu David Maraga kumshauri rais Uhuru Kenyatta kufanya hivyo, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria itakayoruhusu idadi kubwa ya wanawake bungeni.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya raia wawili wa nchi hiyo kuwalisha kesi ya kuitaka Mahakama kuzuia ushauri huo ambao ukitekelezwa Uchaguzi mpya utafanyika baada ya miezi mitatu.

Katiba ya Kenya inataka sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia bungeni kutotawala katika nyadhifa za uteuzi, na kwa miaka 10 sasa wabunge ambao wengi ni wakiume, wameshindwa kupitisha sheria hiyo.

Hatua hiyo ya Jaji Mkuu inaungwa mkono na chama cha Mawakili nchini humo na idadi kubwa ya wabunge wanawake ambao ni asilimia 22 katika baraza la bunge la kitaifa na asilia 22 katika Bunge la Senate.

Rais wa chama cha Mawakili nchini humo, (LSK) Nelson Havi, ametaka rais kulivunja bunge hilo.

Jaji Maraga alisema wabunge na maseneta wamekwenda kinyume cha Katiba ya mwaka 2010 iliyowataka kutunga sheria hiyo.