RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Mpinzani na shujaa wa filamu 'Hotel Rwanda', Paul Rusesabagina, akubali kuunda kundi la waasi

Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi.
Paul Rusesabagina amekuwa akihusishwa kushirikiana na kundi la FNL ambalo mwaka 2018 lilishambulia Kusini mwa nchi hiyo karibu na nchi jirani ya Burundi. AFP/Stringer

Shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda, Paul Rusesabagina, aliyeokoa zaidi ya watu 1,200 wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, amekiri kuwa alishiriki katika kuunda kundi la waasi, lakini amekataa kuhusishwa katika uhalifu wao.

Matangazo ya kibiashara

Paul Rusesabagina ametoa kauli hiyo leo Ijumaa wakati mahakamani imekuwa ikisikiliza kesi yake ya rufaa akipinga uamuzi wa mahakama ya awali aliponyimwa dhamana.

"Tuliunda kundi la FLN kama tawi la kijeshi, na sio kama kundi la kigaidi kama avanvyosema mwendesha mashtaka. Sijakataa kwamba FLN ilifanya uhalifu, lakini jukumu langu mimi lilikuwa la kidiplomasia, "amesema Paul Rusesabagina.

"Katika makubaliano ambayo tulisaini kuunda MRCD, kama chama cha kisiasa, tuliafikiana kuunda tawi la kijeshi liitwalo FLN. Lakini jukumu langu lilikuwa kufanya kazi kwa chama hiki cha siasa na nilikuwa nikisihusika na masuala ya kidiplomasia." , ameongeza mpinzani huyu wa utawala wa rais wa Rwanda Paul Kagame, raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Rwanda kulingana na binti yake.

Baada ya miaka kadhaa akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji na Marekani, Bwana Rusesabagina alikamatwa mwishoni mwa mwezi Agosti na polisi wa Rwanda katika mazingira tatanishi wakati alikuwa safarini huko Dubai.

Alipofikishwa nchini Rwanda alishtakiwa katikati ya mwezi Septemba kwa makosa ya ugaidi, mauaji na ufadhili wa kundi la waasi.

Mnamo mwaka wa 2018, Paul Rusesabagina alianzisha Chama cha MRCD, kinachoshukiwa kuwa na tawi la kijeshi, National Liberation Front (FLN), kundi linalochukuliwa kuwa la kigaidi na serikali ya Kigali.

Mara kadhaa, Bwana Rusesabagina alielezea hadharani kuunga mkono kundi la FLN lakini haijabainika wazi uwezekano wa kuhusika kwake katika kundi hili la waasi, ambalo tayari limefanya mashambulizi kadhaa kwa kutumia silaha kwenye ardhi ya Rwanda, bado.

"Hotel Rwanda" inaelezea jinsi Bwana Rusesabagina, Mhutu aliyeoa mwanamke Mtutsi, mwaka 1994 aliokoa watu zaidi ya 1,200 waliokuwa awlipewa hifadhi katika Hoteli ya Mille Collines huko Kigali, ambapo alikuwa mkurugenzi, akitumia ushawishi wake kwa wanamgambo wa Kihutu, Interahamwe, kutoka chama tawala wakati huo cha MRND.