KENYA-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Wakenya wasubiri kuona masharti zaidi yanalegezwa

Wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini humo wanaona kuwa, huu ni wakati wa uchumi wa nchi hiyo kufunguliwa tena baada ya wizara ya afya kusema kuwa maambukizi yamepungua.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini humo wanaona kuwa, huu ni wakati wa uchumi wa nchi hiyo kufunguliwa tena baada ya wizara ya afya kusema kuwa maambukizi yamepungua. REUTERS/Thomas Mukoya

Rais wa kenya Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kulihutubia taifa hilo mapema wiki hii kuhusu janga la maambukizi ya virusi vya Corona, ambavyo kufikia leo Jumatatu, vimewaathiri watu 38,115 baada ya watu wengine 244 kupatikana na maambuzi hayo kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Wakenya wanasubiri kusikia kwa rais Kenyatta kuhusu ni lini shule zitafunguliwa baada ya walimu kuagizwa kurudi katika maeneo yao ya kazi kuanzia leo Jumatatu

Wachambuzi wa masuala ya uchumi nchini humo wanaona kuwa, huu ni wakati wa uchumi wa nchi hiyo kufunguliwa tena baada ya wizara ya afya kusema kuwa maambukizi yamepungua.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.