TANZANIA-SIASA-USALAMA

Wananchi wa Tanzania wajiandalia Uchaguzi Mkuu

Rais anaye maliza muda wake Tanzania, John Pombe Magufuli.
Rais anaye maliza muda wake Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Sadi Said

Tarehe 28 mwezi ujao, wapiga nchini Tanzania watafanya maamuzi kumchagua rais wao mpya, huku ushindani mkali ukionekana kuwa kati ya mgombea wa chama tawala cha CCM, John Pombe Magufuli, na Tundu Lissu wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA.

Matangazo ya kibiashara

Joto la uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupanda ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya uchaguzi wake wa tano tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Wakati zoezi la kampeni za uchaguzi mkuu likiendelea baadhi ya vyama vya siasa vimesema vimeshuhudia baadhi ya mabango na picha zao kuchafuliwa huku baadhi ya maeneo vikilalamikia bendera zao kushushwa

Hayo yanajiri wakati Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania imemtaka mgombea wa urais kupitia Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu,  kufika mbele ya kamati ya maadili ya taifa kutoa ushahidi kuhusu madai kuwa Tume hiyo inapanga kumwibia kura.

Mkurugenzi wa Tume hiyo Wilson Charles amesema kuwa Tume hiyo imesikitishwa na taarifa za Lissu na kusema ni za uongo kuwa mgombea wa chama tawala CCM rais John Magufuli, mwishoni mwa wiki iliyopita, aliitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi jijini Dodoma kwa lengo la kuhujumu Uchaguzi huo.

Mbali na Tume ya Uchaguzi, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini humo, imemwita Lissu kwa kile inachosema anataoa matamshi yanayohatarisha usalama na amani ya nchi hiyo.

Lissu ameendelea kusisitiza kuwa hatakubali kuibiwa kura, katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 28 Oktoba.