KENYA-UFARANSA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Rais wa Kenya ziarani nchini Ufaransa kuhitimisha mikataba muhimu ya kiuchumi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akipeana mikono na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa hafla katika Kituo Kikuu cha Reli cha Nairobi jijini Nairobi, Machi 13, 2019, siku ya kwanza ya ziara ya kiserikali nchini Kenya.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto) akipeana mikono na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa hafla katika Kituo Kikuu cha Reli cha Nairobi jijini Nairobi, Machi 13, 2019, siku ya kwanza ya ziara ya kiserikali nchini Kenya. Yasuyoshi CHIBA / AFP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anazuru Ufaransa kwa ziara ya siku tano nchini humo. Ziara inayojikita katika masuala nyeti ya kibiashara.  

Matangazo ya kibiashara

Rais Uhuru Kenyatta, ambaye anaambatana na mawaziri watano, atahudhuria mkutano wa benki ya uwekezaji wa umma, atakutana na wafanyabiashara wakuu wa Ufaransa na kusaini mikataba kadhaa.

Uhuru Kenyatta anaambatana na ujumbe mkubwa wa mawaziri na anatarajiwa kuhudhuria hafla kadhaa za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na mkutano katika makao makuu ya BPI France, taasisi inayohusika na kukuza makampuni ya Ufaransa nje ya nchi, lakini pia mkutano huko Medef, makao makuu ya chama cha wafanyabiashara wakuu wa Ufaransa. Ziara hii itapelekea mikataba kadhaa ya karibu Euro Bilioni mbili kusainiwa, chanzo kutoka ikulu ya Élysée kimebaini.

Mwezi Machi 2019, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizuru Kenya, ikiwa ni ziara ya kwanza rasmi ya rais wa Ufaransa nchini Kenya tangu nchi hiyo kupata uhuru. Marais hao wawili walijikubaliana kuhusu miradi kadhaa ya miundombinu. Licha ya China kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Kenya, Ufaransa inavutiwa na nchi hii ya kimkakati ambayo ukuaji wake umeiweka kwa miaka kumi katika kundi la nchi za kipato cha kati.

Miradi mitatu mikuu ya miundombinu

Wakati umewadia sasa wa kutekeleza makubaliano haya kuwa ya kweli, duru za kidiplomasia zimesema. Paris inatarajia kukamilisha mradi wa ujenzi wa barabara kuu inayounganisha mji wa Nairobi na Nakuru na Mau Summit. Mkataba wenye thamani ya Euro Bilioni 1.6. Barabara hii muhimu hutumiwa na malori ya bidhaa zinazoingizwa kutoka pwani. Mazungumzo magumu kwa sababu ya utofauti juu ya hatari ya kigaidi, kawaida huzingatiwa, katika aina hii ya mkataba, na nchi huru. Lakini Nairobi haitatamani kuchukua hatari hii. Kwa hivyo itakuwa mada ya mazungumzo mengine.

Mradi mwingine ni ujenzi wa reli kati ya mji mkuu wa Kenya na uwanja wa ndege. Paris tayari imeandaa makubaliano ya ufadhili wa ukarabati wa reli ya zamani iliyopo, inabaki kusainiwa kwa thamani ya euro milioni 130.