KENYA-UFARANSA-USHIRIKIANO-UCHUMI

Ziara ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini Ufaransa yalenga kuimarisha uchumi

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa ziara yake Paris Oktoba 1, 2020.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa ziara yake Paris Oktoba 1, 2020. REUTERS/Gonzalo Fuentes/Pool

Rais wa nchi ya Kenya ambaye anazuru Ufaransa, ameandamana na ujumbe mkubwa wa mawaziri wake watano katika ziara hii inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta akiandamana na mwenyeji wake Emmanuel Macron, ameshiriki katika mkutano wa Benki ya Uwekezaji wa Umma, taasisi inayohusika na kukuza makampuni ya Ufaransa katika nchi za kigeni.

Wawili hao walitumia fursa hiyo kujadili masuala ya uchumi yanayowaunganisha, licha ya mgogoro wa kafya duniani.Uhuru Kenyatta ameyataja matatizo yanayosababishwa na mgogoro wa Covid-19, "lakini ulimwengu lazima uendelee kujikwamua, lazima tuendelee kusonga mbele, " amebaini rais wa Kenya. Ni vita vinavyoihusu dunia, amekumbusha rais wa Kenyatta, na kuongeza kuwa, hakuna nchi inayoweza kufanya hivyo peke yake, na kwa hilo, lazima kuwepo ushirikiano wa wote ili kujenga Afrika thabiti kwa ajili ya vijana na vizazi vijavyo.

"Mara nyingi tunalitazama bara la Afrika kwa maliasili yake: almasi, mafuta, gesi… na tunakuwa na kitu fulani cha kufumbia macho kwa yale yanayotokea Afrika: Watu, wanawake kwa wanaume wanao uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa ulimwengu bora kwa sote, ”amesema Uhuru Kenyatta.

Mbele ya wafanyabiashara wa Ufaransa, kiongozi huyo amewahakikishia: Tuna wakaribish nchini Kenya. Kwa upande wake, Rais Emmanuel Macron hakuweza kuficha kilichokuwa moyoni mwake kwa nchi hiyo. "Lango limefunguliwa kwa kanda nzima".

"Kwetu, hii ni muhimu sana kwa sababu tunaweza kuwa tumezoea kuwa na mikataba ya mikubwa ya kila mara na wadau wale wale wa katika nchi zile zile za Afrika. Na hiyo sio nzuri. Hii sio nzuri kwa nchi za Afrika na sio nzuri kwetu. Kwa sababu sio hivyo tunavyotaka kuendeleza ushirikiano. Sio jinsi ambavyo tunavyotoa picha ya Ufaransa ilio sahihi. Sio jinsi tunavyotoa majibu ambayo ni muhimu zaidi kwa ujasiriamali, vijana na maendeleo ya Afrika, "amesema rais wa Ufaransa.

Ziara ya Uhuru Kenyatta nchini Ufaransa ni ya siku tano. Anatarajia hasa kukutana na chama cha wafanyabiashara wakuu nchini Ufaransa, MEDEF.