KENYA-RUTO-SIASA-USALAMA

Chama cha Jubilee chaendelea kukumbwa na mpasuko, William Ruto mashakani

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa na naibu wake William Ruto baada ya kutangaza kuundwa kwa chama kipya cha Jubilee Kenya State House

Kamati inayosimamia shughuli za chama tawala cha Jubilee nchini Kenya, inapendekeza naibu rais William Ruto ambaye pia ni naibu kiongozi wa chama hicho, aondolewe katika nafasi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada Ruto na wabunge zaidi ya 30 wanaomuunga mkono siku ya Alhamisi kuvamia makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi na kuendeleza harakati za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2022.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amemshutumu bwana Ruto kwa kuwa 'mjeuri, mwenye madharau na asiyemheshimu Rais Uhuru Kenyatta".

Chama cha Jubilee kimegawayika kati ya wale wanamuunga mkono naibu rais Ruto na rais Uhuru Kenyatta, mpasuko ulioshuhudiwa baada ya maelewano kati ya Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.