RWANDA-UN-KABUGA-HAKI

Majaji watakaosimamia kesi ya Kabuga wateuliwa

Majaji hao ni pamoja na Lain Bonomy raia wa Scotland, Graciela Susana Gatti Santana raia wa Uruguay na Elizabeth Ibanda-Nahamya raia wa Uganda kusimamia kesi hya Kabuga.
Majaji hao ni pamoja na Lain Bonomy raia wa Scotland, Graciela Susana Gatti Santana raia wa Uruguay na Elizabeth Ibanda-Nahamya raia wa Uganda kusimamia kesi hya Kabuga. UNIRMCT/twitter.com

Mahakama ya umoja wa mataifa ilioko jijini Arusha Tanzania imewateua majaji watatu watakaosimamia kesi ya mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda Felicien Kabuga.

Matangazo ya kibiashara

Majaji hao ni pamoja na Lain Bonomy raia wa Scotland, Graciela Susana Gatti Santana raia wa Uruguay na Elizabeth Ibanda-Nahamya raia wa Uganda kusimamia kesi hya Kabuga.

Haya yanajiri baada ya siku ya Jumamatano, mahakama ya Ufaransa kuunga mkono Kabuga kushtakiwa katika mahakama ya Umoja wa mataifa iliopo Arusha.

Félicien Kabuga anadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa Wahutu wenye itikadi kali ambao waliuwa watu 800,000 mwaka 1994.

Félicien Kabuga ni mfanyabiashara maarufu nchini Rwanda, ambaye alichukuliwa kuwa mtu tajiri zaidi nchini humo kabla ya kufanyika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Alizaliwa katika eneo la kaskazini mwa Rwanda ambako alijilimbikizia mali kutokana na biasahara ya majani ya chai miaka ya 1970 na kuwekeza katika biashara tofauti nchini humo, mataifa jirani na ng'ambo.

Alikuwa mwandani wa karibu wa chama tawala cha MRND na baba mkwe wa rais Juvénal Habyarimana.

Kabuga anayetuhumiwa kuwa mfadhili mkuu wa mipango ya kutekeleza mauaji ya kimbari , alikuwa mwenye hisa mkuu katika kituo cha radio ya kibinafsi RTLM ambacho kililaumiwa kwa kuwahamasisha watu wa jamii ya Kihutu kuwaua wenzao wa Watutsi.

Kutokana na utajiri wake, baada ya mauaji ya kimbari Kabuga, mwenye umri wa miaka 84, alifanikiwa kujificha katika mataifa mengi hadi alipokamatwa Mei 16,2020.