RWANDA-RUSESABAGINA-HAKI

Rwanda: Kesi kubwa yatangazwa dhidi ya Paul Rusesabagina na wanachama wa FLN

Mpinzani wa Rwanda Paul Rusesabagina alipowasili katika Mahakama ya Nyarugenge huko Kigali, Oktoba 2, 2020.
Mpinzani wa Rwanda Paul Rusesabagina alipowasili katika Mahakama ya Nyarugenge huko Kigali, Oktoba 2, 2020. AFP Photos/Simon Wohlfahrt

Mwendesha mashataka nchini Rwanda anatarajiwa kuungaisha kesi inayomkabili Paul Rusesabagina, kwa kuhusika katika mapigano ya kimbari ya mwaka wa 1994  na kesi ya waasi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii, mwanasheria mkuu alitangaza kwamba anataka Paul Rusesabagina, shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda, kushtakiwa pamoja na wanachama wa FLN, kundi lenye silaha lililotekeleza mashambulizi kadhaa nchini Rwanda.

Upande wa mashtaka unabaini kwamba ni vyema kuunganisha faili 19, zote zikiwa zinahusiana moja kwa moja au la na mashambulizi yaliyofanywa mnamo mwaka 2018 katika mkoa wa Nyungwe, mashambulizi ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la FLN.

Aimable Havugiyaremye,Mwanasheria mkuu wa Serikali amesema: "Tunawashikilia wapiganaji 16 wa uni la FLN, na tunataka kuwasilisha mashtaka ya pamoja kwa washtakiwa hawa na Paul Rusesabagina. Pia tutaomba kesi hizi ziunganishwe na ile ya Callixte Nsabimana na Herman Nsengimana. Tunaamini kwamba washtakiwa wote 19 watashtakiwa kwa wakati mmoja. "

Callixte Nsabimana, kwa jina maarufu Sankara, ni msemaji wa zamani wa kundi la FLN. Alikamatwa mwaka wa 2019 katika mazingira tatanishi wakati alikuwa akiishi nje ya Rwanda. Familia yake ilidai kwamba alitekwa nyara wakati huo, kama vile Paul Rusesabagina leo. Mamlaka nchini Rwanda zimekanusha madai haya mawili.

Kwa kuunganisha faili hizi, mwendesha mashtaka anachukulia kwamba shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda alikuwa na jukumu la uongozi ndani ya FLN, madai yanayokanushwa na washirika wake wa kisiasa wanaojumuika katika mungano wa upinzani wa MRCD, ulioko uhamishoni. FLN ni tawi la kijeshi la MRCD na Paul Rusesabagina ni mmoja wa vigogo wa MRCD.

Mwanasheria mkuu wa Serikali amebaini kwamba ushahidi uliokusanywa wakati wa msako katika makazi ya Paul Rusesabagina nchini Ubelgiji utawasilishwa wakati wa kesi hiyo, pia akibaini kuwepo kwa ushirikiano kati ya mahakama ya Ubelgiji na ile ya Rwanda katika suala hili.