KENYA-USALAMA

Madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara nchini Kenya mwaka 2019 waachiliwa

Mji wa Mandera unapatikana Kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia na Ethiopia.
Mji wa Mandera unapatikana Kaskazini mwa Kenya kwenye mpaka na Somalia na Ethiopia. Google Maps

Vyanzo kadhaa rasmi, pamoja na Wizara ya Mambo ya nje ya Cuba, vimethibitisha kuachiliwa kwa madaktari wawili wa Cuba. Assel Herrera na Landy Rodriguez walitumwa Mandera, kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka wa Somalia mwaka 2018.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi Aprili 2019, wakati walikuwa njia kuelekea kazini, madaktari hao walitekwa nyara na wanamgambo wa kundi kutoka Somalia la Al Shabab. Mlinzi aliuawa wakati wa utekaji nyara.

Madaktari hao wawili walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu 100 wa afya wa Cuba waliotumwa nchini Kenya mwezi Juni 2018 baada ya makubaliano ya afya yaliyosainiwa kati ya Nairobi na Havana.

Miongoni mwa madaktari waliokuwa kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa x-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva.

Wamekuwa wakitoa huduma na kushauriana na madaktari wengine katika maeneo tofauti nchini Kenya.