KENYA-KENYATTA-SIASA-USALAMA

Rais wa Kenya Kenyatta aendelea kushinikizwa kuvunja bunge

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, alimshauri rais Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Senete, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili.
Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, alimshauri rais Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Senete, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili. PSCU .jpg

Chama cha wanasheria nchini Kenya pamoja na makundi kadhaa ya kupigania haki na demokrasia, yamempa rais Uhuru Kenyatta hadi kufikia 12 ya mwezi huu ili awe amelivunja bunge kwa kuzingatia ushauri wa Jaji Mkuu David Maraga.

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na mjadala ikiwa rais Kenyatta alivunje bunge au kutafuta suluhu nyingine kuhusu suala lililoibua utata wa kikatiba kuhusu theluthi mbili ya wanawake katika uongozi.

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga, alimshauri rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta, kulivunja bunge la kitaifa na lile la Senete, baada ya wabunge kushindwa kupitisha sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili.

Katiba ya Kenya inataka sheria hiyo kuwepo ili kudhibiti jinsia bungeni kutotawala katika nyadhifa za uteuzi, na kwa miaka 10 sasa wabunge, ambao wengi ni wakiume, wameshindwa kupitisha sheria hiyo.

Jaji Maraga alilaumu wabunge na maseneta wamekwenda kinyume cha Katiba ya mwaka 2010 iliyowataka kutunga sheria hiyo.

Hata hivyo Spika wa bunge Justin Muturi ameendelea kupingana na hoja hiyo akisema kwamba kuvunjwa kwa bunge ni chaguo lisilowezekana. Katiba mpya ya Kenya ilizinduliwa 2010, na sheria ya jinsia kuhusu theluthi mbili ilifaa kuidhinishwa baada ya miaka mitano.