TANZANIA-KENYA-CORONA-AFYA-USHIRIKIANO

Coronavirus: Magufuli awataka raia wake kuungana na Wakenya kwa maombi

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS/Emmanuel Herman

Rais wa Tanzania John Magufuli amewataka raia wa nchi yake kuungana na wananchi wa nchi jirani ya Kenya, kwenye maombi ya siku tatu kuliombea taifa hilo dhidi ya maambukizi dhidi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Kenya kwa sasa ina maambukizi zaidi ya Elfu 40 na rais Uhuru Kenyatta alitangaza siku tatu za maombi kuanzia siku ya Ijumaa na leo ataongoza maombi hayo katika Ikulu ya Nairobi.

Rais Magufuli akizungumza katika kampeni ya kisiasa jijini Dar es salaam amewaambia Watanzania, kama walivyomwomba Mungu, waungana na Wakenya ili ugonjwa huo uwaondoke.

Tanzania iliacha kutanagza hali ya maamnbikizi ya Corona mwezi Aprili, na baadaye rais Magufuli kutanagza kuwa baada ya maombi, Mungu alikuwa ameiponya nchi hiyo dhidi ya Corona.