RWANDA-CORONA-AFYA

Rwanda yarekodi vifo 30 kutokana na janga la COVD-19

Rwanda imeanza kulegeza vizuizi dhidi ya Corona.
Rwanda imeanza kulegeza vizuizi dhidi ya Corona. Simon Wohlfahrt / AFP

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Rwanda kutokana na janga la Corona sasa imefikia 30. Nchi hiyo ina maambukizi zaidi ya Elfu nne mia nane, huku watu wengine zaidi ya Elfu wakiwa wamepona.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati watalam kutoka Shirika la Afya duniani, WHO, wanatoa wito kwa serikali za mataifa ya bara Ulaya, kuchukua hatua zaidi kukabiliana na janga la Corona, baada ya maambukizi kuonekana kuongezeka kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Watalaam hao wanapendekeza mikusanyiko ya watu kuzuiwa na hata watu kuiziwa kutembea.

Miongoni mwa mataifa ambayo yanashuhudia ongezeko kubwa la mamabukizi haya ni Ufaransa ambayo siku ya Ijumaa iliripoti visa Elfu 20 kwa siku moja.