KENYA-UCHUMI-KILIMO

Kenya hatarini kuvamiwa tena na nzige wa jangwani

Kenya, mtu huyu akiwa katika wingu la nzige wa jangawani waliovamia shamba lake, karibu na Nanyuki (kaunti ya Laikipia). Februari 2020
Kenya, mtu huyu akiwa katika wingu la nzige wa jangawani waliovamia shamba lake, karibu na Nanyuki (kaunti ya Laikipia). Februari 2020 REUTERS/Baz Ratner

Pembe la Afrika bado linakabiliwa na uvamizi wa nzige wa jangwani. makundi mapya ya nzige wa jangwani yanatarajiwa nchini Ethiopia na Somalia katika wiki zijazo. Kisha wataenea hadi Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo (FAO) limeonya.

Matangazo ya kibiashara

Pembe la Afrika linatishiwa na uvamizi mbaya wa nzige wa jangwani baada ya ule wa miaka 70 iliyopita. Mabilioni ya nzige ambao walivamia kanda hii mwaka huu, wakiharibu makumi ya maelfu ya hekta za mazao, wamezaliana tena.

Nzige wa kike hutaga mayai zaidi ya mia moja kwa wastani. Kwa hivyo watoto wanaotoka kwenye mayai hayo wanaweza kuongezeka mara 20 kila miezi mitatu. Mabuu, ambayo yamefikia hatua ya kukomaa kwa kuanza kuruka, sasa yanaunda makundi haya mapya.

Tayari wameonekana nchini Yemen na Kaskazini mashariki mwa Ethiopia. Mwishoni mwa mwezi Oktoba, watakuwa wamevamia Ethiopia mashariki na Somalia ya kati. Halafu, kaskazini mwa Kenya itakumbwa tena mnamo mwezi Novemba.Wimbi hili jipya linatokana na upepo mkali kutoka Yemen ambao ulienea juu ya Pembe la Afrika, ukibeba mawingu haya makubwa meusi ya mabilioni ya nzige wa jangwani.

Kwa uvamizi wa kipekee wa nzige wa jangani uliorekodiwa mwaka huu tayari umeharibu maelfu ya hekta za mazao na malisho katika Pembe la Afrika, na kusababisha shida kubwa ya chakula. Joto pamoja na mvua kubwa mwishoni mwa mwaka 2019 hadi Februari 2020 ni chanzo cha hali hiyo, FAO imeonya.

Kuna suluhisho moja tu la kushinda tatizo hili: kunyunyizia dawa wadudu. Shughuli za anga na ardhini, ambazo tayari zinaendelea kwa miezi kadhaa, imesema FAO.