TANZANIA-SIASA-USALAMA

Uchaguzi nchini Tanzania: Rais John Magufuli kupambana na wagombea 14

Tanzania's President John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, file.
Tanzania's President John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, file. REUTERS/Emmanuel Herman

Oktoba 28, Watanzania watachagua rais wao mpya na wabunge. Rais wa sasa John Magufuli anawania muhula wa pili. Tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2015, amekuwa akituhumiwa kuongoza nchi kwa ubabe, lakini upinzani unajiandaa kushiriki uchaguzi huo wakati umegawanyika.

Matangazo ya kibiashara

Katika uchaguzi wa urais wa Novemba 28, John Magufuli atachuana na wagombea 14 wa upinzani. Miongoni mwao, Tundu Lissu, mpinzani wake mkuu, mgombea wa chama cha Chadema. Mwaka 2017, Tundu Lissu aliponea chupuchupu kuuawa. Baada ya kupigwa risasi 16 nyumbani kwake katika mji mkuu wa Dodoma na baada ya kufaniwa matibabu na kupona kwa muda mrefu nchini Ubelgiji, mwishowe alirudi nchini Tanzania mwezi Julai mwaka huu.

Mfumo wa ukandamizaji

Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mwishoni mwa mwezi Agosti, Tundu Lissu amekusanya wafuasi wengi kwenye mikutano yake. Lakini mapema mwezi huu, tume ya uchaguzi ilisitisha kampeni yake kwa wiki moja ikimdhtumu kutoa "matamshi ya uchochezi".

John Magufuli anatuhumiwa kuweka mfumo wa ukandamizaji unaozidi kuwa wa kimabavu tangu aingie madarakani. Walakini mgawanyiko wa wapinzani kwa uchaguzi ujao unaweza kumpelekea anashinda tena uchaguzi.

Katika uchaguzi uliotangulia, miaka mitano iliyopita, muungano wa upinzani ulipata kura ambazo hazujawahi kupata katika historia ya nchi hiyo: 40% ya kura. John Magufuli alishinda kwa 58% ya kura. Chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiko madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru mnamo mwaka 1961.Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani Novemba 2015, ameendelea kufanya vizuri katika sekta ya uchumi, maendeleo, vita dhidi ya ufisadi. Na tangu mwaka 2016 vongozi nchini Tanzania wameendelea kujikita hasa katika uchaguzi ujao na wamechukua hatua kali dhidi ya haki za binadamu.