BURUNDI-HAKI ZA BINADAMU

Hali ya wasiwasi yatanda Burundi baada ya mbunge wa zamani wa upinzani kukamatwa

Juni 13, 2020, Rais mteule Evariste Ndashimiye atia saini kitabu cha wazi cha rambirambi kwa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia, Juni 8.
Juni 13, 2020, Rais mteule Evariste Ndashimiye atia saini kitabu cha wazi cha rambirambi kwa mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia, Juni 8. Tchandrou NITANGA / AFP

Nchini Burundi, mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu nchini humo na yale ya kimataifa yanalaani kukamatwa na kufungwa jela kwa mbunge wa zamani wa upinzani, Fabien Banciryanino, Oktoba 2.

Matangazo ya kibiashara

Fabien Banciryanino alikamatwa bila kibali chochote kutoka polisi au ofisi ya mashitaka na kisha kufungwa katika jela kuu la Mpimba jijini Bujumbura wiki iliyopita, akishtumiwa "uasi, kashfa dhidi ya kiongozi na kutaka kuhatarisha usalama wa taifa".

Lakini, kulingana na mmoja wa wanasheria wake na kulingana na barua ambayo mbungr huyo wa zamani alituma kwa CNIDH, Tume Huru ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Burundi na ambayo RFI imepata kopi, aliulizwa maneno aliyotoa wakati wa kikao cha Bunge, mmwezi Februari 2020, alipokuwa bado mbunge.

Fabien Banciryanino alikuwa mmoja wa wakosoaji wakuu wa utawala wa katika bunge lililomaliza muda wake hivi karibuni.

Katika kikao hicho muhimu cha Februari 2020, Bunge la kitaifa lilipitisha muswada uliomuinua na kmumpa cheo rais wa wakati huo Pierre Nkurunziza kuwa "Kiongozi Mkuu wa Uzalendo."

Siku hiyo, Fabien Banciryanino ndiye mbunge pekee aliyetamka hadharani kupinga uamuzi huo. Wakati huo alielezea "uhalifu mkubwa uliotekelezwa kwa miaka 15 ya utawala wa rais Pierre Nkurunziza", ambaye kwa sasa ni marhemu.

Spika wa Bunge wakati huo Pascal Nyabenda alimtuhumu mbunge huyo na kusema kuwa "madai yake hayana msingi".

Mbunge huyo wa zamani amekuwa akihofia usalama wake tangu muhula wake ulipomalizika miezi miwili iliyopita. Siku kumi baada ya kukamatwa kwake, shirika la haki za binadamu ITEKA lilishutumu ukiukaji mkubwa wa Katiba. "Kukamatwa kwa Fabien Banciryanino ni ukiukaji mkubwa wa sheria, hasa kwa kuwa Katiba ya Burundi, katika Ibara ya 155, inasema kwamba hakuna mbunge anayeweza kushtakiwa kwa maoni aliyotoa au pendekezo alilolitoa katika kikao cha bunge, alifanya kazi katika kutekeleza agizo lake ”, amebaini Anschaire Nikoyagize, kiongozi wa ITEKA, akihojiwa na Esdras Ndikumana, wa kitengo cha RFI Afrique.