Coronavirus: Visa vipya 602 vya maambukizi vyathibitishwa Kenya
Imechapishwa: Imehaririwa:
Maambukizi ya virusi ya Corona nchini Kenya, yanaoenkana kuaza kuongezeka tena wiki hii baada ya watu wengine 602 kupatikana na maambukizi hayo kwa kipindi cha saa 24 zilizopita.
Wizara ya afya inaoya kuwa huenda kukawa na mlipuko wa pili wa maambukizi hayo ambayo yamewaathiri watu zaidi ya Elfu 43.
Licha ya onyo hilo na hata shule kufunguliwa wiki hii, Wakenya wameonekana kutozingatia tahadhari inayotolewa na watalaam wa afya na badala yake wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Aidha, wanasiasa wakiongozwa na naibu rais William Ruto wanaendelea na mikutano ya hadhara na kuwakutanisha idadi kubwa ya watu ambao wengi hawavalii barakoa.
Wiki hii Katibu mkuu katika wizara ya afya nchini Kenya, Rashid Aman, alisema kuwa Kenya haipo tayari kwa wimbi lingine la COVID-19.
Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.