TANZANIA-ZANZIBAR-ACT-UCHAGUZI-SIASA

Maalim Seif Sharif Hamad apigwa marufuku kufanya kampeni Zanzibar kwa muda wa siku 5

Mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad
Mgombea urais Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad ACT WAZALENDO ZANZIBAR/twitter.com

Kamati ya maandali ya Tume ya Uchaguzi visiwani Zanzibar nchini Tanzania, imemfungia mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad, kutoafanya kampeni kwa muda wa siku tano kuanzia leo.

Matangazo ya kibiashara

Katibu wa Tume hiyo ya Maadili Khamis Issa Khamis amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya mgombea huyo kuwataka wafuasi wake kujitokeza kwa wingi tarehe 27 mwezi Oktoba kupiga kura, siku ambayo imetengewa maafisa wa usalama kushiriki katika zoezi hilo.

Uchaguzi nchini Tanzania, huko Bara la Visiwani umepangwa kufanyka tarehe 28.

Mbali na visiwani Zanzibar, kampeni zimeshika kasi Tanzania bara, huku rais John Magufuli akipambana na mgombea mkuu wa upinzani Tundu Lissu, kutafuta ushindi wa kuongoza Jamhuri ya muungano wa Tanzania.