TANZANIA-MAFURIKO-MAJANGA ASILI

Mafuriko Tanzania: Kumi na wawili wafariki dunia Dar es salaam

Athari ya mafuriko katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania April 16 2018
Athari ya mafuriko katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania April 16 2018 http://www.mwananchi.co.tz/

Watu Kumi na wawili wamepoteza maisha kufuatia mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha wiki hii jijini Dar es salaam nchini Tanzania kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Polisi imesema watu hao waliangalia baada ya kusombwa na maji kutokana na mafuriko makubwa ambayo pia yamesabisha uharibu wa miundo mbinu kama barabara na mkaazi ya watu huku Wilaya ya Ilala ikiathirika zaidi.

Mafuriko makubwa yamekuwa yakitokea jijini Dar es salaam wakati mvua kubwa inaponyesha katika eneo hilo la Pwani.

Hayo yanajiri wakati serikali kupitia Waziri wa ke wa Utalii Dkt Hamis Kigwangala, ilitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto katika Mlima Kilimanjaro.

Hata hivyo Jumatano wiki hii Waziri Kigwangala alibaini kwamba moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.

Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka Katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.