BURUNDI-NDADAYE-HAKI

Burundi yaadhimisha miaka 27 tangu kutokea mauaji ya Melchior Ndadaye

Rais wa kwanza wa Burundi aliyechaguliwa kidemokrasia, Melchior Ndadaye, aliuawa Oktoba 21,1993.
Rais wa kwanza wa Burundi aliyechaguliwa kidemokrasia, Melchior Ndadaye, aliuawa Oktoba 21,1993. ANP/AFP Dabrowski

Burundi inaadhimisha Jumatano hii Oktoba 21 kumbukumbu ya miaka 27 tangu kuuawa rais Melchior Ndadaye, kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Melchior Ndadaye rais wa kwanza, kutoka jamii ya Wahutu, aliyechaguliwa katika misingi ya kidemokrasia aliauawa usiku wa Octoba 21 mwaka 1993 na kundi la wanajeshi kutoka jamii ya Watutsi wenye msimamo mkali ambao walishindwa kuvumilia kuona mtu kutoka jamii ya Wahutu akiongoza nchi hiyo, iliyotawaliwa na Watutsi kwa miaka zadi ya 31.

Melchior Ndadaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Julai mwaka 2003 dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo,Pierre Buyoya chini ya chama chake cha SAHWANYA -FRODEBU. Ndadaye hakupata muda wa kuongoza nchi hiyo kwani miezi mitatu tu baadaye aliuawa, na hivyo kuzuka machafuko ya kikabila nchini humo, yaliosababisha watu zaidi ya laki nane kupoteza maisha huku wengine wakiitoroka nchi hiyo.

Mkataba wa wa amani na maridhiano uliosainiwa jijini Arusha, ndio uliowaleta pamoja kwa mara ya tena Warundi.

Mwaka 2005, Bunge la taifa hilo, lilipasisha sheria inayo mkubali Melchior Ndadaye kama kinara wa demokrasia nchini Burundi.

Kama ilivyokuwa ada, viongozi mbalimbali wa serikali ya Burundi kwa sasa wanahudhuria misa ya kumuombea kiongozi huyo kwenye kanisa la Cathedrale Regina Mundi jijini Bujumbura na sherehe zingine zitaendelea kwenye eneo alipozikwa katika manispaa ya jiji la Bujumbura.

Wakati huo huo Mahakama Kuu nchini Burundi imewahukumia kifungo cha maisha jela viongozi wa zamani 19, akiwemo rais wa zamani Pierre Buyoya, kwa kupatikana na hatia ya kushiriki mauaji dhidi ya rais wa zamani Melchior Ndadaye.