TANZANIA-USALAMA

Polisi ya Tanzania yathibitisha shambulio la IS karibu na mpaka na Msumbiji

Bendera ya kundi la Islamic State (picha ya kumbukumbu).
Bendera ya kundi la Islamic State (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / YOUTUBE

Polisi ya Tanzania imethibitisha kuwa kundi la Islamic State lilitekeleza shambulio katika kijiji cha Kitaya mpakani na Msumbiji. Shambulio hilo lilitokea wiki iliyopita, na kuua watu kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

Tawi la kundi la Islamic State katika ukanda wa Afrika ya Kati limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Video na picha zinaonyesha majengo kadhaa yakichomwa moto, huku washambuliaji wakiinua sauti wakisema "Allah Akbar" na huku wakimkata kimya mtu mmoja. Shambulio hilo lilidaiwa mapema Oktoba 15 na kundi la IS. Mkurugenzi Mkuu wa Polisi Simon Sirro amethibitisha taarifa hii.

“Ni kweli, wiki iliyopita magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walishambulia kijiji cha Kitaya. Walipora na kuua watu kadhaa. Tuliwafuata na kufanikiwa kuwakamata wachache, ambao wengine ni Watanzania. Lakini ningependa kuhakikishia wananchi kama ninavyosema kila wakati: ukimuua Mtanzania, tutapambana vikali”.

Kijiji cha Kitaya kiko mpakani na Msumbiji. Uasi wa kijihadi unaendelea katika mkoa wa mpakani kwa upande wa Msumbiji tangu mwaka 2017.

Kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Msumbiji na Umoja wa Mataifa, mzozo huu wa kusalama tayari umesababisha kifo vya watu zaidi ya 2,000 na kusababisha watu zaidi ya 300,000 kuyatoroka makaazi yao.

Eneo hili ni la kimkakati kwani kilomita zaidi ya 30 na upande wa Tanzania ni kunapatikana mitambo ya gesi. Shambulio hili pia linatokea siku chache kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 28.