TANZANIA-USALAMA-SIASA

Tanzania: Upinzani washushia lawama Tume ya Uchaguzi kwa kukipendelea chama tawala

Rais wa Tanzania John Magufuli, mgombea kwenye kiti cha urais kwa muhula wa pili, ahutubia wafuasi wake jijini Dar es Salaam, Oktoba 14, 2020.
Rais wa Tanzania John Magufuli, mgombea kwenye kiti cha urais kwa muhula wa pili, ahutubia wafuasi wake jijini Dar es Salaam, Oktoba 14, 2020. Presidential Press Service/Handout via REUTERS

Nchini Tanzania, upinzani unaishtumu Tume ya Uchaguzi nchini humo kwa kupanga kuiba kura kwa kukipendelea chama tawala cha CCM. Hayo yanajizi wakati sikisalia siku tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Wakati Tume ya Uchaguzi mara nyingi inatuhumiwa kwa kukipendelea chama tawala, upinzani unashutumu kwa kuandaa udanganyifu halisi kabla ya uchaguzi huu, kupitia Daftari la wapiga kura.

Freeman Mbwoe, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, ameshutumu kwenye akaunti yake ya Twitter akibaini kwamba kumepangwa udanganyifu mkubwa kupitia Daftari la wapiga kura, akinyooshea lawama Tume ya taifa ya Uchaguzi.

"Mamilioni ya wapiga kura hewa na vituo bandia vya kupigia kura viliongezwa kwenye orodha, wakati wapiga kura kutoka kambi ya upinzani wamehamishwa vituo vya kutazama" amesema Freeman Mbowe.

Wakati huo huo kiongozi wa chama kingine cha upinzani, ACT-Wazalendo Zitto Kabwe pia amethibitisha kwenye ujumbe wa Twitter kwamba karibu wapiga kura 14,000 waliongezwa kwenye Daftari la wapiga kura katika mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa nchi, ambapo alichaguliwa kama mbunge.

Madaia haya yanatolewa kuelekea mwisho wa kampeni ya uchaguzi ambayo haikuwa rahisi kwa upinzani. Kwa mfano, mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Tume ya Uchaguzi ilisitisha kwa wiki moja kampeni ya mgombea wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu, ikimtuhumu kwa "kutoa matamshi ya uchochezi na kuandaa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya sheria za uchaguzi", bila kutoa ushahidi.

Rais John Magufuli, mgombea kwa muhulu wa pili kwenye kiti cha urais, anatuhumiwa kwa kuweka utawala "wa kimabavu" nchini Tanzania wakati wa muhula wake wa kwanza. Lakini, licha ya miaka hii mitano ya ukandamizaji, upinzani unaendelea kuwa na wafuasi wengi.

Kiongozi wa chama cha CHADEMA ameomba katika ujumbe wa Twiter ufafanuzi kutoka Tume ya Uchaguzi na ameonya dhidi ya vurugu kutokea nchini Tanzania.