RWANDA-ICTR-KABUGA-HAKI

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Félicien Kabuga azuiliwa Hague

Félicien Kabuga, anashukiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, hapa akioneshwa kwa mfano wa katuni akiwa mbele ya mahakama Mei 20, 2020.
Félicien Kabuga, anashukiwa kuwa mfadhili wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, hapa akioneshwa kwa mfano wa katuni akiwa mbele ya mahakama Mei 20, 2020. REUTERS/Benoit Tessier

Mfadhili wa mauaji ya kimbari ya Rwanda na mfanyabiashara Félicien Kabuga ambaye alikamatwa katikati ya mwezi Mei baada ya kujificha kwa miaka 26 anakabiliwa na mashtaka saba ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Septemba, Mahakama ya juu nchini Ufaransa ilithibitisha waranti wa kukamatwa uliyotolewa dhidi yake na kuagiza kupelekwa katika kitengo cha mahakama ya kimataifa kinachohusika na kesi za hivi karibuni za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu nchini Rwanda (ICTR), ambayo ilifunga milango yake mwaka 2014.

Mahakama hiyo ina vitengo viwili, moja nchini Tanzania na kingine nchini Uholanzi. Mara tu alipofika katika gereza la Scheveningen, aliwekwa karantini.

Félicien Kabuga amelala usiku wake wa kwanza Jumatatu hii jioni, Oktoba 26, katika gereza la Scheveningen. Mfanyabiashara huyo wa Rwanda anatarajiwa kuzuiliwa kwa siku kumi kabla ya kukutana na majirani zake wapya: viongozi wa kisiasa wa zamani na wa kijeshi wa Serbia Radovan Karadzic na Ratko Mladic, waliohukumiwa na Mahakama ya kimataifa kwa Yugoslavia ya zamani.

Pia siku kumi kabla ya kufikishwa kwake kwa mara ya kwanza mahakamani , ambapo atasema ikiwa ana hatia ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu au la.