Tanzania yafanya Uchaguzi Mkuu katika hali ya mvutano
Imechapishwa:
Wapiga kura zaidi ya milioni 29 wanapiga kura Jumatano hii, Oktoba 28 kwa uchaguzi wa urais, wabunge na serikali za mitaa. Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu saa 7 asubuhi vitafungwa saa kumi alaasiri (saa za Afrika Mashariki).
Siku ya uchaguzi inawadia baada ya kumalizika kwa siku 63 za kampeni.
Kulingana Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage, wapiga kura milioni 29.188 wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la NEC na 566,352, wamejiandikisha katika Daftari la Kudumu la Tume ya Uchaguzi Zanzubar (ZEC).
Wagombea 15 ndio wanawania kiti cha urais katika uchaguzi huo wenye mvutano mkubwa kati ya upinzani na chama tawala.
Rais anaye maliza muda wake John Magufuli, aliyechaguliwa mwaka 2015, anawania katika uchaguzi huu kwa muhula wa pili. Uchaguzi huu unafanyika, wakati vikosi vya usalama na ulinzi vimetumwa katika maeneo mbalimbali kuimarisaha usalama zaidi.
Tayari Jumanne wiki hii makabiliano makali yaliripotiwa katika Visiwa vya Zanzibar, ambapo upinzani umeshtumu polisi kwamba iliua watu kumi na kuwazuia wengi zaidi ya mia moja.
Wakati huo huo Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kimestumu jeshi kwa jaribio la udanganyifu. Hayo yanajiri wakati mgombea wa chama hicho huko Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, alikamatwa jana asubuhi katika moja ya vituo vya kupigia kura. Polisi ilithibitisha taarifa hiyo, bila hata hivyo kutoa sababu.
Wapinzani wakuu wa Magufuli ni pamoja na Tundu Lissu wa chama cha Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA na Bernard Membe wa chama cha ACT Wazalendo.