Taarifa maalum kuhusu Uchaguzi Mkuu Tanzania 2020

Bango lililowekwa picha ya  rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kwenye ukuta wa kilomita 24 uliojengwa karibu na mgodi wa tanzanite wa Merelani karibu na Mlima Kilimanjaro, Aprili 11, 2018.
Imehaririwa: 31/10/2020 - 06:24

Wapiga kura zaidi ya milioni 29 wamepiga kura Jumatano hii, Oktoba 28 kwa uchaguzi wa urais, wabunge na serikali za mitaa. Wagombea 15 ndio wanawania kiti cha urais katika uchaguzi huo wenye mvutano mkubwa kati ya upinzani na chama tawala.Rais anaye maliza muda wake John Magufuli, aliyechaguliwa mwaka 2015, anawania katika uchaguzi huu kwa muhula wa pili. Uchaguzi huu umefanyika, wakati vikosi vya usalama na ulinzi vilitumwa katika maeneo mbalimbali kuimarisaha usalama zaidi.