TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi nchini Tanzania: Wapinzani kadhaa wakamatwa baada ya uchaguzi wenye tata

Rais wa Tanzania, John Magufuli, wakati wa hotuba yake kwa wafuasi wake Oktoba 27, 2020, katika mkoa wa Dodoma.
Rais wa Tanzania, John Magufuli, wakati wa hotuba yake kwa wafuasi wake Oktoba 27, 2020, katika mkoa wa Dodoma. AP Photo

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa urais, wabunge na madiwani nchini Tanzania yalianza kutangazwa Alhamisi (Oktoba 29). Wagombea kutoka chama tawala CCM karibu wote wamebuka washindi.

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa kadhaa na wafuasi wao kutoka kambi ya upinzani amekamatwa baada ya kupinga dhidi ya matokeo ambayo wanadai kuwa hawayatambui.

Kimataifa, uchaguzi huo umetiliwa shaka; hasa nchi ya Marekani ambayo imesema kuna mashaka makubwa kuhusu uaminifu wa uchaguzi huo.

Marekani imezitaka mamlaka za Tanzania kushirikiana na wadau mbalimbali kushughulikia kwa uwazi malalamiko yanayotolewa kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 28 mwaka huu.

Siku ya Alhamisi, chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo kilishutumu ukandamizaji wa utawala dhidi ya wafuasi wake. Huko Zanzibar, kiongozi wa chama hicho, naibu kiongozi na wajumbe wa kamati kuu wa ACT-Wazalendo walikamatwa baada ya kutoa wito wa maandamano ya amani dhidi ya udanganyifu wa uchaguzi. Mmoja wao aliripotiwa kupigwa na polisi na kisha kulazwa hospitalini. Mkurugenzi wa kampeni aliripotiwa kukamatwa kwa kimabavu nyumbani kwake.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo Maalim Seif Hamad aliachiwa kwa dhamana.

Wakati huo huo mgombea urais wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, Chadema - Tundu Lissu, ametangaza kutokuyatambua matokeo ya uchaguzi yaliokumbwa na udanganyifu