TANZANIA-EAC-USALAMA-SIASA

Ujumbe wa waangalizi wa EAC: Uchaguzi umefanyika katika mazingira bora

Rais wa zamani Silvestre Ntibantunganya ambaye ndiye Mwenyekiti wa ujumbe wa waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa zamani Silvestre Ntibantunganya ambaye ndiye Mwenyekiti wa ujumbe wa waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki. East African Community/twitter.com

Ujumbe wa waangalizi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umethibitisha kwamba uchaguzi mkuu nchini Tanzania umefanyika katika mazingira mazuri, na kila mpiga kura alikuwa huru kumchagua anayemtaka bila kutishwa wa hofu.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi kutoka jumuiya hiyo, rais wa zamani wa Burundi Sylvestre Ntibantunganya amebaini kwamba katika siku ya kupiga kura vituo vilifunguliwa kwa muda muafaka, masuala ya kiufundi yalifanywa kwa weledi.

Ujumbe huo umepongeza umewapongeza Watanzania kwa busara na ujasiri walioionesha tangu wakati wa kampeni na uchaguzi kwa kuzingatia amani na usalama.

Sylvestre Ntibantunganya amewasifu Watanzania akibaini kwamba wanaipenda nchi yao, licha ya kueko na vyama vingi na kutofautiana kimaoni.

''Ujumbe wa EAC unawapongeza wagombea, vyama vya siasa na wengine wote kuendelea kuimarisha usalama na amani '' , Bw. Ntibantunganya amsema.

Hata hivyo upinzani umeendelea kupinga matokeo ya uchaguzi ukibaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na udanganyifu mkubwa na kuinyooshea kidole cha lawama Tume Huru ya Uchaguzi, NEC.