KENYA-CORONA-AFYA

Kenya yaendelea kukumbwa na maambukizi zaidi

Kuna ripoti kuwa hopsitali mbalimbali zina wagonjwa wengi, hasa katika miji mikuu ya Nairobi, Mombasa na Kisumu na hivyo kulazimu baadhi ya hospitali  za kibinafsi kutenga vitanda zaidi vya wagonjwa hao.
Kuna ripoti kuwa hopsitali mbalimbali zina wagonjwa wengi, hasa katika miji mikuu ya Nairobi, Mombasa na Kisumu na hivyo kulazimu baadhi ya hospitali  za kibinafsi kutenga vitanda zaidi vya wagonjwa hao. AFP / LUIS TATO

Maambukizi ya virusi ya Corona yanaendelea kuongezeka nchini Kenya na kuzua wasiwasi wa kushuhudiwa kwa mlipuko wa pili wa mamabukizi hayo, baada ya kushuhudiwa kwa maambukizi zaidia ya Elfu Moja katka siku za hivi karibuni, kinyume na ilivyokuwa mwezi Julai.

Matangazo ya kibiashara

Ongezeo hili linazua wasiwasi na huenda serikali nchini humo inachukua hatua zaidi, kama ilivyokuwa miezi iliyopita, kujairbu kudhibiti ongezeko la maambukizi hayo.

Idadi kubwa ya maambukizi imekuwa ikishuhudiwa mwezi Oktoba kinyume na ilivyokuwa miezi ya Juni, Julai na Agosti, na sasa idadi ya vifo pia inaongezeka na watu angalau kumi wanapoteza maisha kila siku.

Kuna ripoti kuwa hospitali mbalimbali zina wagonjwa wengi, hasa katika miji mikuu ya Nairobi, Mombasa na Kisumu na hivyo kulazimu baadhi ya hospitali  za kibinafsi kutenga vitanda zaidi vya wagonjwa hao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inajiandaa kuweka kituo maalum cha kuwasaidia wagonjwa.

Siku ya Jumatano rais Uhuru Kenyatta atakutana na mawaziri pamoja na magavana kujadili ongezeko hili baada ya nchi hiyo kufunguliwa mwezi Agosti , ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa shule  na maeneo ya burudani.