TANZANIA-USALAMA-SIASA

John Pombe Magufuli: Uhuru na demokrasia vina mipaka

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amebaini kwamba uhuru na demokrasia vina mipaka, na kuwatolea wito raia, kila mmoja kuheshimu uhuru wa mwengine, shirika la habari la AFP limeripoti

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli aliyechaguliwa tena kwa muhula wa pili. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

"Lengo la uhuru na demokrasia ni kuleta maendeleo, sio machafuko ...".

Uhuru, haki na demokrasia huenda sambamba na uwajibikaji, na kila mtu ana mipaka.

Natumai kwamba nimeeleweka vyema ", kulingana na rais Magufuli, aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo rais wa Tanzania amezindua shughuli za bunge jipya.

Kauli hiyo inakuja wiki chache baada ya rais kuibuka mshindi kwa asilimia 84 ya kura katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Chama chake, CCM, kiilijinyakulia viti karibu vyote katika Bunge. Upinzani ulidai kuwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania uligubikwa na udanganyifu mkubwa. Hata hivyo Tume ya uchaguzi imeendelea kukanusha madai hayo ya upinzani.