KENYA-CORONA-AFYA

Wahudumu wa afya waendelea kupoteza maisha kutokana na Corona Kenya

Kenya inaendelea kukumbwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.
Kenya inaendelea kukumbwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona. REUTERS/Njeri Mwangi

Wakenya waghabishwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na janga la Corona hasa miongoni mwa wahudumu wa afya baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita, Madktari wawili maarufu nchini humo kupoteza maisha, wakati huu wahudumu wa afya zaidi ya Elfu moja wakiwa wameambukizwa.

Matangazo ya kibiashara

Daktari bingwa wa upasuaji Nira Patel na Anthony Were Omollo ndio madkatari wawili waliopoteza maisha hivi punde kutokana na janga la Covid-19 baada ya wenzao wengine karibu 30 kuangamia tangu kuzuka kwa virusi hivyo mwezi Machi nchini Kenya.

Viongozi wa wahudumu wa afya wamekasirishwa na ongezeko la vifo vya wenzao na wanailaumu serikali kwa kushindwa kuwalinda na kuwapa vifaa vya kujikinga kwa miezi kadhaa sasa na hivyo kuwafanya kufanya kazi katika mazingira magumu, wakati huu wagonjwa wa Corona wanapoendelea kuongezeka.

Madaktari na wahudumu wengine wa afya sasa wanataka kulipwa marupurupu ya kuafanya kazi katika mazingira hatari na kupewa vifaa vya kutosha kuwalinda, la sivyo watagoma kuanzia tarehe sita mwezi Desemba.

Mlipuko wa pili wa Covod-19 umesabisha ongezeko la maambukizi hayo, huku watu zaidi ya 1400 wakipoteza maisha.