UGANDA

Uganda: Museveni apongeza vikosi vya usalama kwa kuzingatia amani, upinzani walalama

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema hatakubali wahalifu kuharibu amani ya nchi hiyo, baada ya siku kadhaa zilizopita maafisa wa usalama kumkatama mgombea wa urais kupitia chama cha upinzani cha NUP Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Rais wa Uganda, Yuweri Museveni.
Rais wa Uganda, Yuweri Museveni. Ug.gov
Matangazo ya kibiashara

Museveni ameunga mkono kukamatwa kwa Kyagulanyi na wafuasi wake na kuwaunga mkono maafisa wa usalama waliokabiliana na wafuasi wa upinzani na kusababisha vifo vya watu 54.

Hata hivyo, Bibi Wine amemshtumu rais Museveni kwa kuendelea kuwalenga wafuasi wake na kukanusha kuwa, anafadhiliwa na raia wa kigeni.

Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Januari, zimekabiliwa na vurugu baada ya maafisa wa usalama kuwazuyia wagombea wa upinzani kwa madai ya kukiuka masharti ya wizara ya afya kukabiliana na mamabukizi ya Corona.

Tayari umoja wa Ulaya na Marekani, wameeleza wasiwasi wao kuhusu uchaguzi wa mwakani, wakionya kuhusu uwezekano wa kutokea vurugu pamoja na namna vyombo vya usalama, vimekuwa vikikabiliana na wanasiasa wa upinzani.

Hivi karibuni rais Museveni, pia alinukuliwa na vyombo vya habari vya nchini mwake, akiwakashifu wanasiasa wa upinzani, akisema wazi haamini kama upinzani una nguvu wa kumuondoa au kuwaletea maendeleo wananchi.

Ujumbe wa Ulaya pia ulisema hautatuma waangalizi wake katika uchaguzi wa mwakani.