BURUNDI-TANZANIA

Tanzania yanyooshewa kidole kuwafanyia dhulma wakimbizi kutoka Burundi

Kundi la wakimbizi wa Burundi, wakiwa katika eneo la Nemba.
Kundi la wakimbizi wa Burundi, wakiwa katika eneo la Nemba. Laure Broulard/RFI

Maafisa wa usalama nchini Tanzania waliwazuia kwa nguvu, kuwatesa na kuwapoteza wakimbizi 18 wa Burundi tangu mwaka 2019 waliokuwa wanaishi katika kambi mbalimbali katika mkoa wa Kigoma, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema hatima ya wakimbizi hao haijulikani na kuna hofu kuwa wakimbizi wengine kutoka Burundi huenda walipitia dhulma hizo.

 

Tanzania imekuwa ikitoa hifadhi kwa wakimbi wa Burundi wapatao 150,000 waliokimbilia nchini humo tangu mwaka 2015 baada ya mzozo wa kisiasa wakati wa utawala wa aliyekuwa rais hayati Pierre Nkurunziza.

 

Serikali ya Tanzania na Burundi, hazijazungumzia kuhusu ripoti hii.

 

Gitega na Dodoma walikuwa wakihimiza wakimbizi wa Burundi waliokimbilia nchini Tanzania kurudi nyumbani wakisema amani imerejea na hakuna sababu za kuendelea kuishi ukimnizini nchini humo.

 

Duru kutoka Burundi zinasema wakimbizi kadhaa walirejea nchini kwa hiari yao, na wengine bado wanaendelea kurejea kutoka nchi jirani ya Rwanda.