Wabunge waliofukuzwa katika chama cha CHADEMA kukata rufaa
Imechapishwa:
Wabunge 19 wa viti maalumu waliovuliwa uanachama wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania , wamesema wataendelea kuwa 'wanachama wa hiari' wa chama hicho, huku wakipanga kukata rufaa juu ya adhabu waliopewa.
Kauli ya wabunge hao imekuja baada ya kuapishwa na baadaye kuvuliwa na Kamati kuu ya chama hicho, ambayo ilisema haikuwakilisha majina ya wabunge hao kwenda bungeni.
Freeman Mbowe ameainisha mapungufu ya kisheria aliyosema yako dhahiri katika mchakato wa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu
Chama cha CHADEMA kinatarajiwa kujibu kauli za wabunge hao.
Mapema wiki hii Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa onyo kwa wale wanaodharau na kukebehi shughuli za Bunge.
"Wako rafiki zetu ambao hivi karibuni wamejipambanua kwa kukejeli shughuli za bunge, niwatahadharishe na kuwakumbusha labda wamesahau kuwa ni jambo lisilokubalika kwa mtu yoyote kudharau shughuli za bunge, kudhalilisha bunge, kudhalilisha uongozi wa bunge na hata kudhalilisha wabunge waliokwisha kuapishwa, “alisema spika la bunge la Tanzania.