UGANDA-BOBI WINE-UCHAGUZI UGANDA 2021

Bobi Wine, atangaza kuendelea na kampeni

Kinara wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyangulanyi, maarufu kama Bobi Wine, hapa ilikuwa wakati akiwasilisha fomu za kuomba uteuzi jijini Kampala, tarehe 21 Agosti 2020.
Kinara wa upinzani nchini Uganda, Robert Kyangulanyi, maarufu kama Bobi Wine, hapa ilikuwa wakati akiwasilisha fomu za kuomba uteuzi jijini Kampala, tarehe 21 Agosti 2020. SUMY SADURNI / AFP

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda ambaye pia ni mgombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani, Robert Kyagulani, maarufu kama Bobi Wine, amesema ataendelea tena na kampeni zake baada ya kuzisitisha kwa siku moja kwa kile alichosema anahofia usalama wake.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana na viongozi wa tume ya uchaguzi siku ya Jumatano, Bobi Wine, amesema alitaka tume ijue kuwa analengwa na vyombo vya usalama.

 

Ameitaka tume ya uchaguzi ihakikishe kuwa vyombo vya usalama vinaheshimu haki yake kutafuta kura.

 

Jana Jumatano Robert Kyagulanyi alishinda siku kutwa katika makao makuu ya tume ya uchaguzi kwa ajili ya kuwasilisha lawama za namna wanavyohujumiwa na kunyanyaswa na vyombo vya usalama.

 

Jumanne wiki hii Bobi Wine alisitisha kampeni zake baada ya walinzi wake wawili na wafuasi kadhaa kujeruhiwa mjini Jinja.

 

Wakati huo huo baadhi ya wafuasi wa chama chake wamependekeza uchaguzi uahirishwe wakidai kuwamba mazingira ya sasa si salama kwa zoezi huru na la amani la kidemokrasia nchini Uganda.