KENYA-MGOMO-MADAKTARI

Covid-19 nchini Kenya: Madaktari watishia kufanya mgomo

Wahudumu wa afya nchini Kenya
Wahudumu wa afya nchini Kenya REUTERS/Baz Ratner

Madaktari pamoja na wahudumu wengine wa afya nchini Kenya wametishia kufanya mgomo katika siku za hivi karibuni, ikiwa madai yao hayatapatiwa suluhu.

Matangazo ya kibiashara

Wahudumu hao wa afya walitarajiwa kuanza mgomo wao leo Jumatatu kabla ya kusitisha hatua yao hiyo, wanadai kwamba serikali haiwalindi vya kutosha dhidi ya ugonjwa hatari wa COVID-19. Wanaomba uwezo zaidi, malipo ya ziada.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu huo Nairobi, Sébastien Németh vyama vya Wauguzi pamoja na wahudumu wengine wa afya vimeamua kutoa nafasi ya mwisho kwa mazungumzo.

Jumapili hii jioni, wauguzi pamoja na wahudumu wengine wa afya, wameamua kusitisha mgomo wao ambao wangelianza leo Jumatatu, wakionya kwamba ikiwa madai yao hayatasikilizwa, wataanza mgomo Desemba 21.

Mgomo huu unakuja wakati mbaya kwa Kenya, wakati kiwango cha vifo 1,500 kutokana na virusi vya Corona kimevuka, huku idadi ya kila siku ya wagonjwa ikivunja rekodi mwishoni mwa mwezi Novemba.
 

Zaidi ya watu elfu moja wamelazwa hospitalini na kuweka mashakani uwezo wa Kenya wa kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa COVID-19. wakati sikukuu za Krismasi na mwaka mpya zikikaribia.

Tayari nchini Kenya madaktari bingwa 10 na wauguzi zaidi ya 30 wamefariki duni kutokana na Covid-19.