BURUNDI-UN-SIASA-USALAMA

Mashirika ya haki za binadamu yaelezea wasiwasi wao kuhusu haki za binadamu nchini Burundi

Evariste Ndayishimiye rais wa Burundi
Evariste Ndayishimiye rais wa Burundi AFP Photos/Tchandrou Nitanga

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya haki za Binadamu leo Alhamisi, Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yametoa wito kwa kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama kuendelea kuangazia maswala na hali ya usalama nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Wito huu unajiri siku chache baada ya kamati hiyo kutangaza kuwa hali ya usalama kwenye nchi hiyo imeanza kuwa nzuri chini ya utawala wa rais Evariste Ndayishimiye.

Hatua hii inajiri baada ya majaribio ya kutaka Umoja wa Mataifa kuendeleza uchunguzi zaidi unaohitajika nchini humo kuhusiana na maswala ya kiusalama kulingana na Louis Charbonneau, mkurugenzi wa Human Rights Watch katika Umoja wa Mataifa UN.

Umoja wa Mataifa uliaanza uchunguzi nchini Burundi mwaka wa 2016 kufuatia kudorora kwa hali ya kiusalama ya binadamu baada ya jaribio la kuipindua serikali mwaka moja kabla ya kuteuliwa kwa Pierre Nkurunziza kwa kuwania urais kwa muhula wa tatu , uteuzi uliopingwa vikali na hata maandamano kushuhudiwa.

Tangu wakati huo, Umoja wa Mataifa ulihitajika kutoa ripoti baada ya miezi mitatau kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini humo.

Katika ripoti yake yake hivi punde, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema mauwaji , na hali ya watu kupotea na hata wengine kukamatwa bila sababu bado inaendelea nchini Burundi japokuwa hali ya mabadilko inaonekana chini ya uongozi mpya.

Seriklai ya Burundi haijazungumzia ripoti hiyo , ila imekuwa ikisema baadhi ya ripoti hizo ni za kisiasa.