TANZANIA-SIASA

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema apewa hifadhi nchini Canada

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema, aliyekimbilia nchini Kenya, akijiandaa kuondoka nchini humo kuelekea Canada (09/12/2020)
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Godbless Lema, aliyekimbilia nchini Kenya, akijiandaa kuondoka nchini humo kuelekea Canada (09/12/2020) COURTESY

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini nchini Tanzania, Godbless Lema, amepewa hifadh ya kisiasa nchini Canada.

Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo wa upinzani aliondoka nchini Kenya siku Jumatano alikokimbilia mwezi uliopita baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba katika nchi yake.

Akiwa nchini Kenya, Lema alisema ametishiwa usalama wake na hivyo hakuwa na lingine bali kukimbilia katika nchi hiyo jirani, madai ambayo mafisa wa Tanzania wamekuwa wakikanusha.

Wakili Wake George Wajackoyah amenukuliwa na vyombo vya Habari nchini Kenya, akithibitisha kuwa Lema na família yake, wameelekea nchini Canada.

Lema anakuwa mwanasiasa wa pili wa upinzani baada ya aliyekuwa mgombea urais Tundu Lissu naye kukimbilia nchini Ubelgiji baada ya kudai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini.

Wanasiasa hao wameonekana kuwa wakosoaji wakubwa wa rais John Magufuli ambaye alitangzwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba na sasa anangoza taifa hilo la Afrika Mashairki kwa muhula wa pili.