KENYA-WABUNGE

Kenya: Wabunge kurejesha pesa serikalini

Bunge la Kenya jijini Nairobi
Bunge la Kenya jijini Nairobi Kevin MIDIGO / AFP

Wabunge nchini Kenya watalazimika kurejesha pesa serikali. Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuomba wabunge 416 kurejesha serikalini dola milioni 10.

Matangazo ya kibiashara

Pesa hizi ni posho ya makazi ambayo wamekuwa wakipokea kwa zaidi ya miaka miwili. Msaada wa kifedha ambao walipiga kura kwa maslahi yao, na kuibua mjadala mkubwa nchini.

Kila mbunge atakuwa na mwaka mmoja kulipa zaidi ya dola 24,000, ikiwa ni kiasi kikubwa kutokana na kiwango cha maisha cha Kenya, lakini kinapatikana zaidi kwa viongozi waliochaguliwa.

Miaka miwili iliyopita, wabunge nchini Kenya walipigia kura posho hii ya makazi ili kuongezwa kwa mishahara yao ambayo ni mikubwa, na na kuibua mjadala mkubwa katika mashirika ya kiraia.

Tume inayohusika na masuala ya mishahara ilipeleka kesi hiyo mahakamani. Taasisi hii huru inayohusika na kupanga mishahara ya wafanyakazi wa serikali inachukuliwa vibaya na wabunge wengi nchini Kenya.

Thande Kuria, wakili wa tume hiyo, amesema kwamba hakuna afisa anayeweza kuamua mshahara wake mwenyewe. "Posho hii ni kinyume na katiba, ni batili na haiwezi kukubalika," amesema.

Wabunge wamekuwa wakilalamika kuwa fidia zao hazikuongezwa tangu mwaka 2013 na kwamba wenzao kutoka vipindi vya awali walilipwa vizuri. Hoja ambazo zilikasirisha mashirika mengi yasiyo ya kiserikali.