RWANDA-CORONA

Covid-19: Rwanda kuongeza marufuku ya kutotoka nje wakati wa sikukuu

Wanafunzi nchini Rwanda wakiwa darasani huku wamevaa barakoa
Wanafunzi nchini Rwanda wakiwa darasani huku wamevaa barakoa Simon Wohlfahrt / AFP

Wengi wanajiuliza iwapo Rwanda inakabiliwa na mlipuko wa pili wa ugonjwa hatari wa COVID-19, ambapo katika siku za hivi karibuni, nchi hiyo ilirekodi visa vingi vya maambukizi, ambapo visa mia moja viliripotiwa kwa siku.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu hizi hazikuwahi kurekodiwa nchini humo tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Rwanda, nchi ambayo inaendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya COVID-19.

Serikali, ambayo katika wiki za hivi karibuni ilifungua baadhi ya sekta za uchumi, ilitangaza hatua mpya Jumatatu (Desemba 14) kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo wakati wa sikukuu za mwisho wa Mwaka.

Hakuna maadhimisho katika nafasi za umma, au sherehe katika nafasi za kibinafsi kwa sikuu za mwisho wa Mwaka nchini Rwanda. Mikusanyiko yote imepigwa tena marufuku. Wanyarwanda watalazimika kusherehekea Krismasi na Mwaka Mpya chini ya amri ya kutotoka nje, iliyowekwa kuanzia saa 2 mchana usiku kati ya Desemba 22 na Januari 4.

Ukumbi wa michezo na mabwawa ya kuogelea, ambayo yaliruhusiwa kufungua tena wiki tatu zilizopita, vimetakiwa kufungwa. Na mazungumzo makubwa ya kitaifa ya kila mwaka (Umushyikirano), ymeahirishwa kwa tarehe ambayo haikutangazwa.