KENYA

Serikali ya Kenya yatishia kuwafuta kazi madaktari na wahudumu wa afya wanaogoma

Wahudumu katika Hospitali Kuu ya Kenyatta jijini Nairobi
Wahudumu katika Hospitali Kuu ya Kenyatta jijini Nairobi (AP Photo)

Madaktari nchini Kenya wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kulamamikia kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la virusi vya Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa Madaktari na serikali nchini humo kugonga mwamba.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametishia kuwafuta kazi wahudumu walioamua kugoma.

Mgomo huu unakuja wakati huu nchi nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na mlipuko wa pili wa  janga la Covid 19 lililoripotiwa nchini humo mwezi Machi.

Kenya imerekodi visa 94,500 vya maambukizi ya virusi vya Corona, huku watu wengine  1,639 wakipoteza maisha.

Watu wengine  75,735 wamepona maambukizi hayo.