KENYA

Serikali ya kenya yatishia kuwafuta kazi madaktari na wahudumu wanaofanya mgomo

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta Yasuyoshi CHIBA / AFP

Madaktari nchini Kenya wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kulamamikia kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la virusi vya Covid-19.

Matangazo ya kibiashara

Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa Madaktari na serikali nchini humo kugonga mwamba.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametishia kuwafuta kazi wahudumu walioamua kugoma.

Mgomo huu unakuja wakati huu nchi nchi hiyo inapoendelea kukabiliana na janga la Corona.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 94,500 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 349 kuthibitishwa na vifo 94,500 baada ya ya watu wengine 6 kuthibitishwa kufariki dunia kutoka na janga hilo hatari la COVID-19.

Watu 176 wameripotiwa kupona virusi hivyo na kufanya idadi ya jumla ya watu waliopona kufikia 75,735.