TANZANIA-BURUNDI

Tanzania: Ipi hatima ya wakimbizi wa Burundi kabla ya tarehe ya mwisho ya Desemba 31

Wakimbizi wa Burundi
Wakimbizi wa Burundi UN Photo/Sebastian Villar

Mwishoni mwa mwezi Agosti 2020, Burundi na Tanzania zilitia saini makubaliano ya kuwataka wakimbizi wa Burundi walioko Tanzania kurudi nyumbani kwao ikiwa ni kwa hiari yao au la kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na moja ya mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali nchini Burundi, karibu watu hamsini kati ya wakimbizi hao walikabiliwa na visa vya unyanyasaji mkubwa na wengine 170 wameripotiwa kutoweka tangu mwaka 2015.

 

Muungano wa watetezi wa haki za binadamu kutoka Burundi wanaoishi katika kambi za wakimbizi wameendelea kulalamikia hali hiyo na kutoa wito kwa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi kuhusu visa hivyo.

 

Shirika hili linadai kuchangia ripoti ya hivi karibuni ya Haki za Binadamu ambayo ilitaja kesi kadhaa za wakimbizi kutoweka katika mazingira tatanishi,  mateso, kuteswa na kufukuzwa kiholeka kwa wakimbizi.

 

Shirika lisilo la kiserikali kutoka Marekani limesema limerekodi visa vya ukiukwaji dhidi ya wakimbizi wasiopungua 18 tangu mwishoni mwa mwaka 2019. Shirika hilo lisilo la kiserikali kutoka Burundi linadai limerekodi karibu watu hamsini ambao walikabiliwa na visa hivyo.

 

Wiki iliyopita, Mwandishi Maalum anayehusika na masuala ya wakimbizi na watafuta hifadhi ya Ukimbizi barani Afrika alilaani na kushutumu shinikizo zinazoongezeka kwa wakimbizi wa Burundi kutoka mamlaka ya Tanzania ikiwataka waondoke nchini humo. Aliitaka mamalaka ya Tanzania kuhakikisha imekomesha visa hivyo vya unyanyasaji.

 

Kati ya mwezi Septemba 2017 na mwisho wa mwezi Oktoba 2019, karibu wakimbizi 79,000 walikuwa wameamua kurudi kwa hiari kwao Burundi chini ya makubaliano kati ya nchi hizo mbili na UNHCR.

 

Takriban wakimbizi 700 walirundi nchini Burundi kutoka Tanzania kila wiki wakati nchi hizo mbili zilitarajia kuwa wakimbizi 2,000 wangelirudi nyumbani kwa wiki.

 

Hata hivyo makubaliano mapya yaliyosainiwa mnamo mwezi Agosti ambayo yanatoa nafasi kwa wakimbi kurudi nyumbani kwa hiari yao au kufurushwa kwa nguvu katika ardhi ya Tanzania, hali inayotia wasiwasi wanaharakati wa haki za binadamu leo.