KENYA

Kenya: Wanafunzi warudi shuleni baada ya kukaa nyumbani kwa muda mrefu

Wanafunzi wa Shule ya msingi nchini Kenya
Wanafunzi wa Shule ya msingi nchini Kenya Farm Images/Universal Images Group via Getty Images

Shughuli zimeanza tena katika shule zote nchini Kenya baada ya serikali kuchukuwa hatua ya kufunga shule katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi tisa ya shule zote kufungwa kwa sababu ya janga la COVID-19, hatimaye wanafunzi milioni 16 wanatarajia kurejea shuleni.

Kufungwa kwa shule nchini Kenya mnamo mwezi Machi 2020, kulikuwa na athari mbaya kwa watoto. Idadi kubwa ya watoto wanatarajia kuacha shule baada ya kusalia nyumbani kwa muda mrefu.

Ni miezi tisa sasa tangu hayua hiyo ichukuliwe, licha ya kuwa baadhi ya shule ziliweka utaratibu wa wanafunzi wao kufuata visomo kwa njia ya intaneti, lakini ni Wakenya wachache tu ndio ambao waliweza kupata vifaa muhimu vya kiteknolojia ili kufuata visomo kwa njia hiyo.

Kufungwa kwa shule kwa muda mrefu ni hatua ambayo iliwashangaza wengi, wakati makanisa, mikahawa na maduka yaliendelea na shughuli mbalimbali tangu kuzuka kwa janga hilo.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wasichana zaidi ya 2 kati ya 5 kwa sasa wana ujauzito nchini Kenya.

Wasichana wadogo walioachwa na wazazi wao wanaendelea kufanya kazi. Baadhi yao waliolewa, bado ni watoto.

Kuna watoto wa mitaani, ambao wanaonekana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi wakiishi kwa kuombaomba. Wengine waliamua kufanya kazi ili kusaidia wazazi wao kukidhi majhitaji ya familia.

Bila kusahau uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya ambao, mambo ambayo yameathiri vijana nchini Kenya.

Watoto wengi, labda mamia ya maelfu, ambao huenda wasirudi shule leo Jumatatu.