UGANDA

Uchaguzi Mkuu nchini Uganda kufanyika siku ya Alhamisi

Mgombea mkuu wa upinzani Bobi Wineakifanya kampeni jijini Kampala
Mgombea mkuu wa upinzani Bobi Wineakifanya kampeni jijini Kampala Reuters

Uchaguzi Mkuu nchini Uganda utafanyika siku ya Alhamisi, wakati huu hofu ikiendelea kutanda kutokana na kampeni nchini humo kutawaliwa na maafisa wa usalama, kuwahangaisha wagombea wa upinzani na wanahabari.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa Uganda unakabiliwa na mtihani mkubwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Tume ya uchaguzi imetoa angalizo kwa wagombea wote kuzingatia taratibu za afya kuepusha kuenea kwa maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.

Rais wa muda mrefu Yoweri Kaguta Museveni ambaye anawania muhula mwingine, anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa hasimu wake kisiasa mgombea wa upinzani Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine.

Yoweri Museveni, aliingia madarakani baada ya kutoka katika mapigano ya msituni mwaka 1986, na anatambulika kuwa kiongozi amedumu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Rais huyo mwenye miaka 76, ameweza kulifanya taifa hilo kuwa na amani kwa muda mrefu na kuleta maendeleo ambayo wengi wanafurahia.

Lakini aliweza kuimarisha utawala wake kwa kuhamasisha utu na ushirikiano , kutoa ajira , kuruhusu kuanzishwa kwa taasisi huru na kuwatenga wapinzani.

Bobi Wine, muimbaji ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, ameendelea kukumbana na changamoto kadhaa na askari.

Mbunge huyo ambaye nyota aliyeweza kuvuta umati mkubwa wa vijana , alikumbana na maswaibu kadhaa katika kampeni zake.

Katika kampeni zake polisi walimkamata na kumfunga, wafuasi wake walipigwa mabomu ya machozi na kupigwa risasi kwa kuwa walikwa wanaenda kinyume na masharti dhidi ya corona.

Wakati wa kampeni , waandamanaji 54 waliuawa wakati Bobi Wine aliposhikiliwa na polisi na wengine wengi wanaaminika kuwa walipiwa risasi.

Miaka 12 iliyopita, Bobi alikuwa akijulikana kwa kuimba nyimbo zinazoeleza maisha ya watu masikini - yeye mwenyewe akiwa amezaliwa na kukulia katika mazingira ya kimasikini huko Kamwokya, na hilo ndilo jambo lililompa umaarufu mkubwa miongoni mwa wananchi wa taifa hilo ambao wengi wao ni masikini.