TANZANIA-MSUMBIJI

Marais wa Msumbuji na Tanzania wakutana, wajadili suala tata la usalama

Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi (Kushoto)  na mwenzake wa Tanzania John Magufuli (Kulia) walipokutana Chato Januari 11 2021
Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi (Kushoto) na mwenzake wa Tanzania John Magufuli (Kulia) walipokutana Chato Januari 11 2021 Youtube

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi alikutana na mwenyeji wake wa Tanzania John Magufuli siku ya Jumatatu na kujadiliana masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizo mbili hasa suala tata la utovu wa usalama katika mpaka wa nchi hizo mbili katika mkoa wa Cabo Delgado kwa upande wa Msumbiji na Mtwara kwa upande wa Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la kijihadi ambalo limekuwa likitekeleza mashambulizi na mauaji katika mkoa wa Cabi Delgado, eneo lenye utajiri wa gesi wamekuwa wakiripotiwa kuvuka eneo la Mtwara na kutekeleza mauaji.

Hata hivyo, viongozi hao wawili hawakuweka wazi mazungumzo yao kuhusu suyala hili la usalama walipozungumza na umma.

Serikali ya Tanzania uliopita, ilituma wanajeshi wake kwenye maeneo ya mpaka ili kudhibiti tishio kutoka nchini Msumbuji.

Mwezi Oktoba mwaka 2020, magaidi hao walishambulia kijiji cha Kitaya huko Mtwara na mkuu wa Jeshi la polisi nchini  Tanzania Simon Sirro alinukuliwa akisema magaidi zaidi ya 300 walivuka mpaka na kufanya uhalifu na mauaji.